Tuesday, 29 July 2014

LEO NI VIZURI KUANGALIA VIDEO HIZI KWA AJILI YA KUJIFUNZA ZAIDI JUU YA MNYAMA HUYU KWA FAIDA ZAKE


Kwa kuwa kuna methali  isemayo kuwa picha huzungumza au uwakilisha maneno elfu nimeona ni vyema tuone jirani zetu wa Kenya walivyojipanga katika kazi hii ya ufugaji  wa wandege hawa, bila kupoteza  muda angalia link hizi hapa chini
Part one video

Part two video

Naamini utakuwa umefurahi video hizi tafadhali embu eleza hapo chini uzoefu wako katika kufunga na kama unapenda kujifunza zaidi kuna wataalamu wengi katika ulimwengu wa kware Tanzania wanaweza kukusaidia.



Karibu na uwe na siku njema.



Visit below links for more information

BENEFIT OF QUAIL EGGS
1.Benefit of Quail EGGS

2.Other healthy benefit

3.Ufumbuzi toka nchi nyingine kuhusu ufugaji wa kware.

Monday, 28 July 2014

Karibu kwenye ulimwengu wa Kware (Quail) au Tomboro








Kware ni mmoja wa ndege wa ajabu sana na anaendela kushangaza kila nisomambo ambapo imenilazimu nijiulize kiumbe hiki  kinachoonyesha kuwa na faida nyingi hivi kwa binadamu asili yake nini, na kwa kuwa  naamini Mungu aliumba kila kitu kwa manufaa ya kumsaidia binadamu ndipo nilipolikuta kumbe kiumbe huyu Mungu aliwaletea kwa mara ya kwanza wanadamu, pale wana wa Israel walipokuwa wanatoka Misri na walikuwa na hamu ya nyama sana  Mungu akawaletea mnayama huyu wamle soma Kutoka 16:13.  na ile Zaburi 105 :40 inayokazia  kwa kusema " Walipotaka akaleta kware, akawashibisha chakula cha mbinguni.
Kwa hiyo kwa maelezo hayo hapo juu huyu ni mmojawapo wa viumbe ambavyo aliviumba Mungu kwa ajili ya binadamu na hivyo vina manufaa muhimu katika mwili wa binadamu.
 Mayai na Umuhimu wake 
Zaidi ya nyama yake ambayo haina mafuta na ni tamu mayai ya kware yamekuwa kirutubisho muhimu sana katika mwili inasaidia sana katika kuweka ufahamu wa mtoto na mtu mzima vyema, inaondoa  lehemu (Cholesterol) iliyombaya mwilini na kuweka ile iliyo nzuri. inaongeza uwezo wa binadamu kumpambana na magonjwa na allegy hasa ya ngozi  inarudi katika hali yake ya kawaida kwa haya ndio mambo niliyo naushahidi nayo kulikuwa na ndugu zangu wamepata stroke wako kitandani na kwenye wheel chair baada ya dawa siku moja daktari akawaambia watafute mayai ya kware ale baada ya  wiki tatu alitoka kwenye wheel chair na mwingine aliyokuwa amelala kitandani  baada ya kutumia mwezi anatembelea fimbo, nilikuwa mtu wakutokubali na kupinga hili kuwa mayai  haya madogo yanaweza kufanya hivi baada ya kupitia kwenye mtandao nikagundua umuhimu wake na kuwafanya watoto wawe na akili nzuri. Nimeona hasa kwenye allergy kuna watoto walikuwa na allergy na baadhi ya vyakula ambavyo wanavipenda sana sasa tulipowapa mayai haya baada ya muda wanakula vyakula hivi bila ya allegy yoyote  na ngozi zao zinaendelea kuwa nyororo.
Nashukuru sana kwa kukutnana na kitu hiki zama hizi tutumie mayai ya kware ni bora na ni matamu.Mara nyingi nimepata maswali haya mayai yanaliwaje ni kama vile unavyokula mayai mengine unaweza kuchemsha, kukaanga na hata kula mabichi, Kwa leo nitaishia hapo mpaka wakati mwingine.Tafadhali angalia hizo links hapo chini kwa faida.

Visit below links for more information

BENEFIT OF QUAIL EGGS
1.Benefit of Quail EGGS

2.Other healthy benefit

3.Ufumbuzi toka nchi nyingine kuhusu ufugaji wa kware.