Monday, 18 May 2015

JINSI YA KUWEKEZA KWENYE UFUGAJI WA KWARE

Nashukuru kuwa ufugaji wa kware unaendelea kupata  wapenzi wengi kutokana na faida kama chakula bora kwa ndege huyu ila kumekuwa na  taarifa nyingi na hasa faida ya kifedha ambayo inaweza kupatikana kutokana na kufuga ndege huyu na vilevile bei ya bidhaa hii imeendelea kuwa juu  sana kiasi kwamba hivi kweli bei hizi za bidhaa hii zina uhalisia kiasi gani. Na kwa kuwa ni kitu kipya katika jamii yetu na mara nyingi watu wanataka kuchukua nafasi ambayo itakuwa rahisi na kuleta hela nyingi kwa mara  moja lakini ukweli kuhusu utajiri unabaki pale pale kuwa inachukuwa  muda na katika kuchukua muda watu wengi wanaachwa wakishangaa na wengine kuona kama aina fulani ya utapeli.
 Leo nimeamua kuweka number kama unataka kufanya ufugaji huu kwa muda mrefu lazima kwanza uangalie uhalisia wake kwa kina na kuona kama bado unahitaji kujiuliza hivi kama  bei za bidhaa hizi zitashuka zaidi ya nusu utaweza kuendelea kuwa na faida na kwa kiasi gani unaweza kuhimili kuwekeza katika biashara hii kama hakutakuwa  na nini malengo na makusudio yako  ukichaweka na kujua hilo ndio uingie kwenye shughuli hii. Kwahiyo kwa kukusaidia nimejaribu kuweka mahesabu hayo kwenye excel sheet ambayo itaweza kukuonyesha  faida unayoweza kupata na kwa mahesabu ya kware 500 unaweza kupata faida ya wastani wa Tshs millioni moja kwa mwezi  kwahiyo unaweza kushusha kutokana na  kiasi unachoweza ingawa unavyoenda chini  inaweza kuwa chini zaidi lakini kwa kware 100 inaweza kukupa kati ya laki moja na nusu  hivi kwa mwezi .
 angalia mahesabu  hapo chini na kama unaswali unaweza kuniuliza na  kama uengependa kujua zaidi unaweza kuweka comment hapo chini


Description/ Maelezo IDADI (Quantity) KIASI (Amount) JUMLA (Total)
1 Gharama ya kununua kware 300 wa wiki moja                500            3,500         1,750,000
2 Chakula kwa muda wa miaka miwili na nusu9 Kware hula gram 30 kwa siku kware 500 hula kilo 15          13,800                160         2,208,000
3 Madawa na utaalamu matumizi ya wiki                130          10,000         1,300,000
5 Ujenzi wa banda la kukaa ngazi tatu mita 3 kwa 1.5                     1       750,000            750,000
6 Gharama za usimazi na wafanyakazi  kwa miezi 30                  30       500,000      15,000,000
7 Dharura na mengineyo  na gharama ya masoko 20% ya gharama zote juu                     1    1,201,600
       1,201,600

Jumla  ya matumizi   22,209,600
Mapato
Kware huanza kutanga vyema baada ya wiki nane  na utakuwa na kware 400 wanaotaga 100 vijogoo na wanataga kwa siku 215 to 250 kwa mwaka  kwa miaka miwili na nusu  kware mmoja atatupa mayai (215*2.5=538) kwa kware wetu 400*538        215,000                250      53,750,000
Baada ya miaka miwili uza kware wako wote                  450            3,000         1,350,000
Ukipata mahali pa kuuza mbolea vile vile itakuwa sawa ila kwenye hili sitaiweka
Jumla ya mapato   55,100,000
Faida tarajiwa  kwa miaka miwili na nusu   32,890,400
Faida kwa mwezi     1,096,347

Friday, 24 April 2015

Mabanda mazuri ya kware ni yapi

Nimekuwa ninapokea email nyingi kuhusu mabanda ya kware yameje ili uweze kufuga kware vyema kwa kuwa watu wengi wanapenda  kuwa na kware kati ya 100 na mia mbili  mambo makuu matatu unatakiwa kuwepo katika mabanda ya kware.
1, Moja kuwe na hewa ya kutosha
2. Sehemu ya kunyea maji  na chakula ili waweze
3. liwe limefunikwa ili kwamba wasiweze kutoka nje maana wao huweza kuruka.

Sasa watu wengine walikuwa wanafuga kuku kwahiyo kama ulishafuga kuku wa kisasa ambao uliweka kwenye banda na kware ni wadogo basi katika square mita moja unaweza kuweka kware 25 mpaka  30   nawakawa kwenye nafasi ya kutosha na kuweka maranda basi unaendelea na ufugaji wako. Ila kwa wale ambao wana sehemu ndogo unaweza kutengeneza cages za ngazi tatu za mita mita mbili kwa moja na nusu nakuwza kware wako 40  kwenye kila ngazi na ukawa nazo nyingi tu  njisi unavyotaka
                                       




    Banda ambalo mbolea inatolewa kwenye vidroo ila kitu cha kuhakikisha unakuwa na umbali wa kutosha ili kware wasiungue   na amonia maana mbolea ya kware ina amonia nyingi


Tuesday, 24 February 2015

UMUHIMU WA MAYAI YA KWARE KATIKA KUPAMBANA NA ALLERGIES NA KUWEKA AFYA YA UBONGO

Siku za karibuni nimendela kupata habari kutoka kwa wateja wangu jinsi gani watu waliokuwa na matatizo ya kiafya hasa ya allergy na kupoteza kumbukumbu walivyosaidika kwenye matatizoa yao. Lakini kwa kuwa mimi sio mwasanyansi ila ni naamini watu waliotangulia wanaweza kuwa wamefanya utafiti zaidi ili nami nipate sehemu ya kuizungumzia kisanyansi na baada ya kuaanza kutafuta nini hasa kimefanyika ndipo nilipokuta  makala ya Dr J. C Truggier, Daktari wa kifaransa ambaye katika miaka ya 1960 aliamua kufanya utafiti baada ya kuona watu wengi waliotumia mayai ya kware wanapata nafuu hasa kwenye allergy za mazingira wanayoishi na wanaume walikuwa wamepungukiwa na nguvu za kiume zikirudi kwa miaka kumi alifanya utafiti na akagundua kuwa mayai haya yanasaidia sana katika kukuza kinga ya mwili wa binadamu kupambana na magonjwa na hivyo hivyo katika kufanya watu wenye allergy mbalimbali kuendelea vyema na kutosumbuliwa na hasa wale waliokuwa wanasumbuliwa na vumbi na hatimaye utafiti wake ulichapishwa katika  French Medical Journal 15 March 1978 ukipenda ujisomee wenyewe kwa urefu hii hapa link yake
file:///C:/Users/user/Downloads/9.Truffier%20JC-1978-EN-Treatment%20of%20allergy-Quail%20eggs.pdf

Ila kiu yangu haikuishia hapo nikaendelea kutafuta tafiti ambazo nazo zimefanyika siku za karibuni ikiwa nayo technologia imeuongezeka ndipo  nilipokutaana na moja iliyochapishwa kwenye  International Journal of Scientific and Research Publication volume 3 ya toleo la tarehe 05 May 2013 ambalo baada ya utafiti wao walifikia hitimisho hili  "
"Many nutrient benefits of quail eggs which most of them as good sources of protein, fat, vitamin E, minerals (nitrogen, iron and zinc) and sex hormone P. Thus, we should educate or transfer knowledge to people for good nutrient benefits of quail eggs as good nutritional foods and may be the alternative resolving problem of people in some or all nutritional nutrients necessary for human health in developing countries and may be a good potential to resolve “World Food Problem”.
ukitaka utafiti wote na jinsi walivyofikia hapo unaweza kuupata kwenye  hii link
http://www.ijsrp.org/research-paper-0513/ijsrp-p1729.pdf
Naamini tukiendelea kutumia mayai yake nakuona faida zake tunaweza kuomba wana sayansi wetu nao wafanye utafiti ili tuendelee kujua faida zake nyinginezo ambazo hazijangundulika bado nawatakieni siku njema.


Friday, 2 January 2015

NAWATAKIENI HERI NA FANAKA ZA MWAKA MPYA



Tunapoingia mwaka mpya 2015 , napenda kuchukua nafasi hii kwanza kabisa kumshukuru Mungu aliyetuwezesha kufika siku ya leo na pili kuwashukuru wateja wote na wafugaji ambao wanaendelea kujifunza zaidi kuhusu umuhimu wa ndege aina ya kware na faida zake katika maisha ya binadamu. Katika mwaka uliopita nimepata kujifunza mengi na nimepokea ushauri mwengi na vile vile shuhuda nyingi ya jinsi mayai ya kware kama chakula bora kilivyowasaidia watu mbalimbali na kama inavyoonyesha ni watu asilimia chini ya 10% wanakuja na kutoa shukrani basi naamini watu wengi zaidi wamenufaika tuendelee kujifunza umuhimu wa chakula hiki katika  afya ya binadamu nawatakiani kila la heri na fanaka tele katika mwaka huu 2015.
Mungu awabariki na kuwalinda wote