Monday, 18 May 2015

JINSI YA KUWEKEZA KWENYE UFUGAJI WA KWARE

Nashukuru kuwa ufugaji wa kware unaendelea kupata  wapenzi wengi kutokana na faida kama chakula bora kwa ndege huyu ila kumekuwa na  taarifa nyingi na hasa faida ya kifedha ambayo inaweza kupatikana kutokana na kufuga ndege huyu na vilevile bei ya bidhaa hii imeendelea kuwa juu  sana kiasi kwamba hivi kweli bei hizi za bidhaa hii zina uhalisia kiasi gani. Na kwa kuwa ni kitu kipya katika jamii yetu na mara nyingi watu wanataka kuchukua nafasi ambayo itakuwa rahisi na kuleta hela nyingi kwa mara  moja lakini ukweli kuhusu utajiri unabaki pale pale kuwa inachukuwa  muda na katika kuchukua muda watu wengi wanaachwa wakishangaa na wengine kuona kama aina fulani ya utapeli.
 Leo nimeamua kuweka number kama unataka kufanya ufugaji huu kwa muda mrefu lazima kwanza uangalie uhalisia wake kwa kina na kuona kama bado unahitaji kujiuliza hivi kama  bei za bidhaa hizi zitashuka zaidi ya nusu utaweza kuendelea kuwa na faida na kwa kiasi gani unaweza kuhimili kuwekeza katika biashara hii kama hakutakuwa  na nini malengo na makusudio yako  ukichaweka na kujua hilo ndio uingie kwenye shughuli hii. Kwahiyo kwa kukusaidia nimejaribu kuweka mahesabu hayo kwenye excel sheet ambayo itaweza kukuonyesha  faida unayoweza kupata na kwa mahesabu ya kware 500 unaweza kupata faida ya wastani wa Tshs millioni moja kwa mwezi  kwahiyo unaweza kushusha kutokana na  kiasi unachoweza ingawa unavyoenda chini  inaweza kuwa chini zaidi lakini kwa kware 100 inaweza kukupa kati ya laki moja na nusu  hivi kwa mwezi .
 angalia mahesabu  hapo chini na kama unaswali unaweza kuniuliza na  kama uengependa kujua zaidi unaweza kuweka comment hapo chini


Description/ Maelezo IDADI (Quantity) KIASI (Amount) JUMLA (Total)
1 Gharama ya kununua kware 300 wa wiki moja                500            3,500         1,750,000
2 Chakula kwa muda wa miaka miwili na nusu9 Kware hula gram 30 kwa siku kware 500 hula kilo 15          13,800                160         2,208,000
3 Madawa na utaalamu matumizi ya wiki                130          10,000         1,300,000
5 Ujenzi wa banda la kukaa ngazi tatu mita 3 kwa 1.5                     1       750,000            750,000
6 Gharama za usimazi na wafanyakazi  kwa miezi 30                  30       500,000      15,000,000
7 Dharura na mengineyo  na gharama ya masoko 20% ya gharama zote juu                     1    1,201,600
       1,201,600

Jumla  ya matumizi   22,209,600
Mapato
Kware huanza kutanga vyema baada ya wiki nane  na utakuwa na kware 400 wanaotaga 100 vijogoo na wanataga kwa siku 215 to 250 kwa mwaka  kwa miaka miwili na nusu  kware mmoja atatupa mayai (215*2.5=538) kwa kware wetu 400*538        215,000                250      53,750,000
Baada ya miaka miwili uza kware wako wote                  450            3,000         1,350,000
Ukipata mahali pa kuuza mbolea vile vile itakuwa sawa ila kwenye hili sitaiweka
Jumla ya mapato   55,100,000
Faida tarajiwa  kwa miaka miwili na nusu   32,890,400
Faida kwa mwezi     1,096,347