Sunday, 24 April 2016

KUANGALIA FAIDA YA UFUGAJI WA KWARE ( PROFIT FORECAST)

Leo nimeona niweke moja ya excel sheet inayoonyesha  jinsi biashara hii inaweza kuwa na faida. Sheet hii nilitengeneza mwaka jana nilipokuwa nafanya forecast zangu wewe unaweza kuadjust kwa kutumia mpango wako. Kwa sasa biashara hii imeshuka ila bado mahitaji yako sokoni hasa kwa wale ambao waliona faida yake na wameweza kuvumilia downward nakushauri fuga kidogo kwa matumizi yako wakati unaangalia jinsi ya kuingia sokoni kivingine. Usiache kufuga ndege wengine ukitegemea hawa tu  maelezo hayo ni kwa kufuga kware  500
 




tion/ Maelezo IDADI (Quantity) KIASI (Amount) JUMLA (Total)  
1 Gharama ya kununua kware 300 wa wiki moja                520            3,500         1,820,000  
2 Chakula kwa muda wa miaka miwili na nusu9 Kware hula gram 30 kwa siku kware 500 hula kilo 15          13,800                160         2,208,000  
3 Madawa na utaalamu matumizi ya wiki                130          10,000         1,300,000  
5 Ujenzi wa banda la kukaa ngazi tatu mita 3 kwa 1.5                     1       750,000            750,000  
6 Gharama za usimazi na wafanyakazi  kwa miezi 30                  30       500,000      15,000,000  
7 Dharura na mengineyo  na gharama ya masoko 20% ya gharama zote juu                     1    1,215,600         1,215,600  
  Jumla  ya matumizi       22,293,600  
           
  Mapato        
  Kware huanza kutanga vyema baada ya wiki nane  na utakuwa na kware 400 wanaotaga 100 vijogoo na wanataga kwa siku 215 to 250 kwa mwaka  kwa miaka miwili na nusu  kware mmoja atatupa mayai (215*2.5=538) kwa kware wetu 400*538        215,000                250      53,750,000  
  Baada ya miaka miwili uza kware wako wote                  450            3,000         1,350,000  
  Ukipata mahali pa kuuza mbolea vile vile itakuwa sawa ila kwenye hili sitaiweka        
  Jumla ya mapato       55,100,000  
           
  Faida tarajiwa  kwa miaka miwili       32,806,400  
  Faida kwa mwezi         1,093,547  
*Angalizo  mahesabu haya yamewekwa   yakiassume kuwa  kware asilimia 4 tu ndio watakufa  na inawezekana kwenye hali halisi ikawa tofauti
Unaweza kuweka comment yako hapo chini tuendelee kujifunza zaidi

Monday, 18 May 2015

JINSI YA KUWEKEZA KWENYE UFUGAJI WA KWARE

Nashukuru kuwa ufugaji wa kware unaendelea kupata  wapenzi wengi kutokana na faida kama chakula bora kwa ndege huyu ila kumekuwa na  taarifa nyingi na hasa faida ya kifedha ambayo inaweza kupatikana kutokana na kufuga ndege huyu na vilevile bei ya bidhaa hii imeendelea kuwa juu  sana kiasi kwamba hivi kweli bei hizi za bidhaa hii zina uhalisia kiasi gani. Na kwa kuwa ni kitu kipya katika jamii yetu na mara nyingi watu wanataka kuchukua nafasi ambayo itakuwa rahisi na kuleta hela nyingi kwa mara  moja lakini ukweli kuhusu utajiri unabaki pale pale kuwa inachukuwa  muda na katika kuchukua muda watu wengi wanaachwa wakishangaa na wengine kuona kama aina fulani ya utapeli.
 Leo nimeamua kuweka number kama unataka kufanya ufugaji huu kwa muda mrefu lazima kwanza uangalie uhalisia wake kwa kina na kuona kama bado unahitaji kujiuliza hivi kama  bei za bidhaa hizi zitashuka zaidi ya nusu utaweza kuendelea kuwa na faida na kwa kiasi gani unaweza kuhimili kuwekeza katika biashara hii kama hakutakuwa  na nini malengo na makusudio yako  ukichaweka na kujua hilo ndio uingie kwenye shughuli hii. Kwahiyo kwa kukusaidia nimejaribu kuweka mahesabu hayo kwenye excel sheet ambayo itaweza kukuonyesha  faida unayoweza kupata na kwa mahesabu ya kware 500 unaweza kupata faida ya wastani wa Tshs millioni moja kwa mwezi  kwahiyo unaweza kushusha kutokana na  kiasi unachoweza ingawa unavyoenda chini  inaweza kuwa chini zaidi lakini kwa kware 100 inaweza kukupa kati ya laki moja na nusu  hivi kwa mwezi .
 angalia mahesabu  hapo chini na kama unaswali unaweza kuniuliza na  kama uengependa kujua zaidi unaweza kuweka comment hapo chini


Description/ Maelezo IDADI (Quantity) KIASI (Amount) JUMLA (Total)
1 Gharama ya kununua kware 300 wa wiki moja                500            3,500         1,750,000
2 Chakula kwa muda wa miaka miwili na nusu9 Kware hula gram 30 kwa siku kware 500 hula kilo 15          13,800                160         2,208,000
3 Madawa na utaalamu matumizi ya wiki                130          10,000         1,300,000
5 Ujenzi wa banda la kukaa ngazi tatu mita 3 kwa 1.5                     1       750,000            750,000
6 Gharama za usimazi na wafanyakazi  kwa miezi 30                  30       500,000      15,000,000
7 Dharura na mengineyo  na gharama ya masoko 20% ya gharama zote juu                     1    1,201,600
       1,201,600

Jumla  ya matumizi   22,209,600
Mapato
Kware huanza kutanga vyema baada ya wiki nane  na utakuwa na kware 400 wanaotaga 100 vijogoo na wanataga kwa siku 215 to 250 kwa mwaka  kwa miaka miwili na nusu  kware mmoja atatupa mayai (215*2.5=538) kwa kware wetu 400*538        215,000                250      53,750,000
Baada ya miaka miwili uza kware wako wote                  450            3,000         1,350,000
Ukipata mahali pa kuuza mbolea vile vile itakuwa sawa ila kwenye hili sitaiweka
Jumla ya mapato   55,100,000
Faida tarajiwa  kwa miaka miwili na nusu   32,890,400
Faida kwa mwezi     1,096,347

Friday, 24 April 2015

Mabanda mazuri ya kware ni yapi

Nimekuwa ninapokea email nyingi kuhusu mabanda ya kware yameje ili uweze kufuga kware vyema kwa kuwa watu wengi wanapenda  kuwa na kware kati ya 100 na mia mbili  mambo makuu matatu unatakiwa kuwepo katika mabanda ya kware.
1, Moja kuwe na hewa ya kutosha
2. Sehemu ya kunyea maji  na chakula ili waweze
3. liwe limefunikwa ili kwamba wasiweze kutoka nje maana wao huweza kuruka.

Sasa watu wengine walikuwa wanafuga kuku kwahiyo kama ulishafuga kuku wa kisasa ambao uliweka kwenye banda na kware ni wadogo basi katika square mita moja unaweza kuweka kware 25 mpaka  30   nawakawa kwenye nafasi ya kutosha na kuweka maranda basi unaendelea na ufugaji wako. Ila kwa wale ambao wana sehemu ndogo unaweza kutengeneza cages za ngazi tatu za mita mita mbili kwa moja na nusu nakuwza kware wako 40  kwenye kila ngazi na ukawa nazo nyingi tu  njisi unavyotaka
                                       




    Banda ambalo mbolea inatolewa kwenye vidroo ila kitu cha kuhakikisha unakuwa na umbali wa kutosha ili kware wasiungue   na amonia maana mbolea ya kware ina amonia nyingi


Tuesday, 24 February 2015

UMUHIMU WA MAYAI YA KWARE KATIKA KUPAMBANA NA ALLERGIES NA KUWEKA AFYA YA UBONGO

Siku za karibuni nimendela kupata habari kutoka kwa wateja wangu jinsi gani watu waliokuwa na matatizo ya kiafya hasa ya allergy na kupoteza kumbukumbu walivyosaidika kwenye matatizoa yao. Lakini kwa kuwa mimi sio mwasanyansi ila ni naamini watu waliotangulia wanaweza kuwa wamefanya utafiti zaidi ili nami nipate sehemu ya kuizungumzia kisanyansi na baada ya kuaanza kutafuta nini hasa kimefanyika ndipo nilipokuta  makala ya Dr J. C Truggier, Daktari wa kifaransa ambaye katika miaka ya 1960 aliamua kufanya utafiti baada ya kuona watu wengi waliotumia mayai ya kware wanapata nafuu hasa kwenye allergy za mazingira wanayoishi na wanaume walikuwa wamepungukiwa na nguvu za kiume zikirudi kwa miaka kumi alifanya utafiti na akagundua kuwa mayai haya yanasaidia sana katika kukuza kinga ya mwili wa binadamu kupambana na magonjwa na hivyo hivyo katika kufanya watu wenye allergy mbalimbali kuendelea vyema na kutosumbuliwa na hasa wale waliokuwa wanasumbuliwa na vumbi na hatimaye utafiti wake ulichapishwa katika  French Medical Journal 15 March 1978 ukipenda ujisomee wenyewe kwa urefu hii hapa link yake
file:///C:/Users/user/Downloads/9.Truffier%20JC-1978-EN-Treatment%20of%20allergy-Quail%20eggs.pdf

Ila kiu yangu haikuishia hapo nikaendelea kutafuta tafiti ambazo nazo zimefanyika siku za karibuni ikiwa nayo technologia imeuongezeka ndipo  nilipokutaana na moja iliyochapishwa kwenye  International Journal of Scientific and Research Publication volume 3 ya toleo la tarehe 05 May 2013 ambalo baada ya utafiti wao walifikia hitimisho hili  "
"Many nutrient benefits of quail eggs which most of them as good sources of protein, fat, vitamin E, minerals (nitrogen, iron and zinc) and sex hormone P. Thus, we should educate or transfer knowledge to people for good nutrient benefits of quail eggs as good nutritional foods and may be the alternative resolving problem of people in some or all nutritional nutrients necessary for human health in developing countries and may be a good potential to resolve “World Food Problem”.
ukitaka utafiti wote na jinsi walivyofikia hapo unaweza kuupata kwenye  hii link
http://www.ijsrp.org/research-paper-0513/ijsrp-p1729.pdf
Naamini tukiendelea kutumia mayai yake nakuona faida zake tunaweza kuomba wana sayansi wetu nao wafanye utafiti ili tuendelee kujua faida zake nyinginezo ambazo hazijangundulika bado nawatakieni siku njema.


Friday, 2 January 2015

NAWATAKIENI HERI NA FANAKA ZA MWAKA MPYA



Tunapoingia mwaka mpya 2015 , napenda kuchukua nafasi hii kwanza kabisa kumshukuru Mungu aliyetuwezesha kufika siku ya leo na pili kuwashukuru wateja wote na wafugaji ambao wanaendelea kujifunza zaidi kuhusu umuhimu wa ndege aina ya kware na faida zake katika maisha ya binadamu. Katika mwaka uliopita nimepata kujifunza mengi na nimepokea ushauri mwengi na vile vile shuhuda nyingi ya jinsi mayai ya kware kama chakula bora kilivyowasaidia watu mbalimbali na kama inavyoonyesha ni watu asilimia chini ya 10% wanakuja na kutoa shukrani basi naamini watu wengi zaidi wamenufaika tuendelee kujifunza umuhimu wa chakula hiki katika  afya ya binadamu nawatakiani kila la heri na fanaka tele katika mwaka huu 2015.
Mungu awabariki na kuwalinda wote

Saturday, 30 August 2014

MAYAI YA KWARE YANALIWAJE





Baada ya kuelimishana juu ya umuhimu wa mayai yak ware katika mwili wa binadamu watu wengi walipitia sehemu mbalilmbali wameona kwenye  mtandao kuwa yana umuhimu kweli kwenye afya zetu  kama chakula bora. Sasa swali ninaloulizwa mara kwa mara ni je yanatumiwaje au yanaliwaje? Mayai ya kware yanaaliwa vilevile kama yanavyoliwa ya kuku unaweza kukaanga, kuchemsha na hata kula  wabichi vyovyote ambavyo wewe utaona inafaa., mimi napenda zaidi kula ya kuchemsha au kuyasteam kwenye mvuke naona hivyo ndio matamu. Mayai haya ambayo mimi napenda kuyaita kuwa super food yanasaidia sana watu katika kuimarisha kumbukumbu, watu wenye kisukari nyama isiponyee, watu wenye shinikizo la damu au pressure na inaondoa cholesterol mbay inaweka nzuri maana mayai yak ware yana cholesterol nzuri kwa asilimia kubwa sana. Hapa chini ni jinsi ya kutumia ukiwa unataka kuweka afya yako vizuri tumia matatu kila siku kwa mtu mzima au mawili kwa watoto walio na umri chini ya miaka 16 kwasababu mayai haya ni madogo matatu ni karibu sawa na yai moja la kuku. Ikiwa unarecover au unasumbuliwa na magonjwa  mbalimbali wakati unatumia dawa ulizoandikiwa sio vibaya ukala chakula hiki bora kama ilivyoainishwa  kwenye  matandao wa http://www.quailfarm.co.uk kwa kufuata siku hizo na mayai hayo  yalioaninishwa hapa chini.
Age Group
Jumlaya mayai ya kware

Total No of Quail Eggs
Jumla ya siku

Total No of Days
Siku ya kwanza

1st Day
Siku ya pili

2nd Day
Siku ya tatu

3rd Day
Kuanzia siku ya nne na kuendelea

From the 4th Day on
Adult/watu wazima
240
49
3
3
4
5
Adult/Watu wazima
120
25
3
3
4
5
16-18 yrs/miaka
120
25
3
3
4
5
11-15 yrs/miaka
120
31
3
3
3
4
8-10 yrs/miaka
90
30
3
3
3
3
4-7 yrs/miaka
60
20
3
3
3
3
1-3 yrs/miaka
60
30
2
2
2
2
3 miezi/mount - 1 yr/mwaka
30
30
1
1
1
1

For Children: The consumption of quail eggs is recommended for children whether cooked or raw for their physical and mental balance. Quail eggs help improving the IQ.

Growth stimulation and metabolism improvement
100eggs
Reactivate the nerves and central nervous system
120eggs
For the elderly: Quail eggs have brilliant regenerative effects on the body therefore are recommended for the elderly. It can calm down and/or cure many diseases attributed to old age, deficiency or excess nutrients in the body.

quail eggs help renewing the state of health and brings the body to equilibrium, combats the degenerative process and rejuvenates the body
240eggs
revives memory and protects nerve cells
120eggs
improves sexual potency
120eggs
reinforces organs weakened by physical work or stress
240eggs
fortifies the body
240eggs
Asthma
240eggs
Skin rash
120eggs
Eczema conjunctivitis
120eggs
Allergic rhinitis
240eggs
Gastric ulcers
240eggs
Poor digestion
120eggs
Excess secretions of stomach acids
120eggs
Improves  liver organ functions
240eggs
Improves the functioning of the heart in the case of coronary sclerosis
240eggs
anaemia
240eggs
arterial hypertension
240eggs
gouts
240eggs
obesity
240eggs
diabetes
240eggs
neurasthenics
240eggs
nervous state
240eggs
Benefits of quail eggs during pregnancy and while breast feeding:

The consumption of quail eggs fortifies the woman’s body during pre and post natal periods as well as after surgery and radiotherapy. It also has beneficial effects on the foetus (physical and mental balance) and for the mother after delivery (physical rehabilitation and rejuvenation of cells). Quail eggs also improve the quality of breast milk.
240eggs
The consumption of quail eggs by HIV AIDS patients improves CD4
240egg