Sunday, 10 August 2014

TOFAUTI ILIYOKO KATI YA MAYAI YA KWARE NA KUKU





Katika siku chache baada ya kupost kuhusu kware hapa kwenye hii page ya  ulimwengu wa kware nimekuwa nikipata maswali kuwa nini hasa tofauti ya mayai ya kware na yale ya kuku ingawa mada za awali zilikuwa zinaonyesha tu kwa habari za watu waliopata kutumia mayai haya na kuona umuhimu wake katika afya na baadhi ya tovuti kuongelea tu kwamba mayai haya ni mazuri yanasaidia kwa afya bado kama watu tulienda shule ilikuwa haikidhi haja kuamani tu yakuwa yana saidia katiaka afya, nikiwa mmojawapo wa watu ambao niliona yanasaidia watu walikuwa nakuoteza kumbukumbukumbu, wenye matatizo ya miguu, pressure, kisukari, rush kwenye ngozi na alleggy wakiendelea vizuri. Na mpaka sasa mimi napenda kuiita hiki chakula bora na sio dawa  kama watu wengi waliotumia wakapata nafuu au kupona ya yaliokuwa yakiwasibu   na wale waliokuwa  na dhaifu nyingine katika mwili wakarejea afya maridhawa lakini msimano wangu binafsi napenda kutambua mchango wake haya mayai kama chakula bora.  Ndio maana hata Mungu aliamua kuwapa wana waisrael kama chakula kwenye Kutoka 16:13 na mtumishi Daudi anakomelezea kwenye Zaburi 105:40. Sasa kwa kuwa siku zote najua kuwa Mungu hapingani na sayansi kitu wanasayansi wanachofanya nikungudua tu mambo ambayo Mungu ameyaweka  kwahiyo ikabidi nitafute kisayansi sasa sisi tunaopenda kuoona na kufanya akili zetu zielewe maana ukielewa jambo kwenye akili  yako ni rahisi kufanyia kazi na kwenda mbele na sio kitu kibaya aliyetuumba anapenda sana tutumie akili zetu.
Katika kutafuta nikasema pamoja na vyanzo vya wataalamu binafsi ningependa kupata vyanzo vilivyo vya kiserekali ambavyo wao hawana upande waliolalia maana hawa wataalamu binafsi wanaweza kuwa na ajenda zao, Na ndipo nilipopata  utafiti wa USDA (United State Department of  Agriculture) unaonyesha tofauti za mayai haya kwa kina katika category 78 za nutrients  zilizogawanya mayai ya kware yana  vitu 31 zaidi ambayo ya kuku hayana kabisa wakati yale ya kuku ya kitu kimoja tu ambacho hakiko kwenye ya kware ambacho naomba nikitaje nacho ni Vitamin K (phylloquinone) na  katika hizo 45 vilivyobaki vya kware 42 viko juu  na vingine hata mara mbili ya zile za kuku, wakati vya kuku ni 3 vitatu  ambayo vimezidi vile vya kware.  Angalia link hizo hapo chini kwa number kamili

1. Bofya hapa ikuonyeshe mlinganisho wa mayai ya  kware na kuku katika nutrients

2. Bofya hapa uone nutrients za mayai ya  kware peeke yake


3.  Bofya hapa uone nutrients za mayai ya kuku peeke yake

Naomba niwakilishe nakaribisha maswali comment hapo chini ili tuendelee kujifunza zaidi faida ya ndege huyu na manufaa yake katika maisha yetu Ahsanteni na karibuni.

No comments:

Post a Comment